JE, WAJUA NAKSHI YA SHANGA ASILI YAKE NI AFRICA.

          ** AFRO FASHION**


       karibu ndugu kwenye safu hii inayo jikita zaidi katika kukufunulia tamaduni za kiafrika kwaundani zaidi juu ya masuala yote ya urembo na mchango wao katika  'fashion' hii leo. karibu!
      WAZULU na WASWAZI wa Afrika Kusini wanatamaduni wa kutengeneza vito vya aina yake na vyenye kuvutia sana. Mapambo (bangili , hereni n.k) hayo hutengenezwa kwa kutumia shanga zifumwazo kwa ustadi wa hali ya juu, shanga hizo zimepatiwa jina la ROCAILLES
              Kwa wazulu huweza kufuma kwa kuweka nakshi za rangi tofauti za shanga hizo kwa makusudio ya kutoa ujumbe fulani ulio kusudiwa. Pia hutolewa na rafiki wa kike kwa mpenzi wake wa kiume kwa makusudio muhususi ;bangili ya shanga za rangi nyekundu humaanisha upendo wa kupindukia kwa mpenziwe, 'moyo wangu unabubujikwa na damu kwa upendo wako'. Shanga za rangi ya njano humaanisha wizu, na nyeusi huelezea hasira na uchungu (moyo wangu umechukizwa kwa usaliti / moyo wangu umepasuka kwa maumivu pindi niliposikia unampenzi mwingine).
          Kwa wahindi wekundu wa Amerika ya kaskazini hutumia mifupa na mbegu maalumu wakitumia na shanga kutengeneza vito vyao. Hakika hustadi huu ni wa kipeke na waaina yake.Tamaduni zao hizo zimekuza sekta ya utali 'tourism' kwa  kuvutia sana wageni toka sehemu mbalimbali na kupiga hodi kwa vijana wanao tafuta ajira hivi leo, jambo hili limewawezesha kujiajiri wenyewe. Zaidi ni pale inapo jitambulisha kwenye 'fashion' hii leo, sasa shanga hizo zatumika na wabunifu wengi wa mavazi ndani na nje ya Afrika na kuitambulisha kama mavazi ya kiafrika, shanga huweza kufumwa kwenye magauni sehemu za shingo/kola, kwenye mikono sehemu ya chini kwa magauni na hata bukta pia kwenye mikanda, kutengeneza hereni, bangili, cheni na hata pete mbalimbali. Hakika ni sana inayovutia sana kwenye macho ya wengi.

0 comments: