Habari wapenzi wa safu hii, kama ifahamikavyo kila mwaka tarehe 14 ya mwezi februari ni siku ya wapendanao VALENTINE DAY. Wengi huumiza kichwa linapokuja suala la zawadi gani yakumzawadia mpenzi wake au yeyote ampendaye ( mzazi, mtoto, rafiki ) siku ya VALENTINE DAY. kuna usemi usemao ' zawadi ni zawadi ', na kweli zawadi ni zawadi; je, ulisha jiuliza zawadi bora ni ipi? Zawadi bora sio lazima iwe ileinayouzwa ghali. Zawadi bora ni ile itakayo furahiwa na kukumbukwa kipindi kirefu hata miaka kadha. Basi chagua kulicho bora kwa mpenzi wako. Zipo njia nyingi ila hizi ni bora zaidi kwako;
Njia ya kwanza ni ya kuangalia akipendacho mwenzi wako na kumpatia kama zawadi. mfano, mpenzi wako anapenda kuogelea basi kumnunulia 'swimsuite' kama zawadi. Ikiwa anapenda michezo basi ni wazo zuri kumnunulia viatu vya michezo ( sport shoes ) kama njumu , nike ____ au waweza mnunulia jezi.
Njia nyingine ni kuangali kitu akipendacho sana ( her/his dream thing). Unaweza kujua akipenda kwa kumfuatili anachopenda kukizungumzia mara nyingi na angependa kukipata. Mfano, kama mpenzi wako anapenda zungumzia 'smartphones' basi ukimnunulia I phone, android phones au windows phones ni vizuri.
Unaweza pia kuangalia kitu akipendacho kukitumia na kimesha chaka au kupitwa na wakati na kumnunuli kipya, kama mpenzi wako anapenda kuvaa saa na ishapitwa na wakati au kuchaka basi kumnunulia mpya kama zawadi ni bora.
Njia nyingine ni kuangalia kipaji chake. mfano anapenda kuchora basi kumnunulia 'set' ya vifaa vya kuchorea huenda ikamfurahisha na akahisi unamjali.
Njia ya mwisho ni kutumia kipaji chako kuanda zawadi kwa mwenzi wako. kama wewe unakipaji cha kuchora basi unaweza mpa zawadi ya picha ulio ichora inaweza.
- ANGALIZO
MAZINGATIO
- 'kama anakupenda atajali zawadi utakayompelekea ili mradi ni kwa ajili ya kumsaidia'
- 'KUJALI AFYA ZETU na MWENZI WAKO JUU YA MAAMBUKIZO YA UKIMWI (HIV/AIDS)'
0 comments: