PLAN B REC. GETTING HOT!

TUFF GIZZLE (OWNER)
        
RED AGAIN (PRODUCER)
PLAN B RECORD, ni studio ya mziki inayokuja kasi tokea pande za kaskazini mwa Tanzania, hapa namaanisha mkoa uliopewa jina la mlima mrefu kuliko yote Afrika. Hapa namaanisha Kilimanjaro, na ukitazama ramani yake hutokosa kuuna mji adhim wa Moshi mjini; ndipo waliweka maskani yao studio za PLAN B. Studio hii yenyelengo laku wainua wasanii wachanga pia imetanua wigo wake na kupokea wasanii wakubwa wa ndani na nje ya Kilimanjaro. Hii imedhihirika baada yakufanya nyimbo ambayo ndani yake Darasa ametia vocal (ipo njiani).
        Bilashaka unakiu yakuifahamu zaidi, PLAN B RECORDS, ilianzishwa mwaka 2010, mwanzo ilifahamika kwa jina la ONE LOVE RECORD, ilianzia Dar es salaam kabla yakuamishiwa Moshi. Studio hizi inamilikiwa na kijana mdogo Shabani Ally al maarufu TUFF GIZZLE. Red Again ndio producer mkuu wa Plan B records, ni producer anayefanya vizuri kwani ametengeneza 'hit and hot songs' zinazotesa kwenye chat mbalimbali za radio pande za kaskazini. Baadhi ya nyimbo zilizofanyika PLAN B RECORDS; sururu ya kaskazini - Sururu, like it - Plan B Crew, Natamani - R.daddy, principal - GOOD ON SPEE ft GENERAL BOY. Na nyingine nyingi zinazotarajiwa kutolewa hivi karibuni ikiwemo aliyoshirikishwa Darasa.
Nilipata kutembelea studio hizi nkapata fursa yakuongea na mmiliki wa studio hizo, tuliongea mengi akanidokezea juu yakufungu VIDEO PRODUCTION siku za usoni. Nilimuliza jinsi gani unawaidia wasani wachanga? alijibu " kwanza gharama zetu ni nafuu na cha zaidi tunasaidia kuitangaza ngoma zao redioni" alimaliza kwa kusema " PLAN B RECORDS tumedhamiria kuteka soko la mziki Tanzania".

Huo ulikua waraka mfupi wa PLAN B RECORDS, kwa habari zaidi tembeleeni studio zao zilizopo PASUA-MATINDIGANI, MOSHI MJINI au official blog yao.
SHUKRANI
Shukrani zangu ziwaende crew na uongozi wa PLAN B RECORDS kwa ukarimu wao na kuifanikisha post hii.
Asanteni wadau wa STREETSWAGGERIFIC

0 comments: